Home

UTARATIBU WA KUCHUKUA TRANSCRIPT/CHETI KWA WALIOMALIZA MASOMO YAO

Wapendwa wateja wetu, tunapenda kuwatangazia utaratibu ufuatao unatakiwa kufuatwa katika  kuchukua transcript na vyeti hapa chuoni Mtwara. Utaratibu huu unatakiwa kukamilika kabla ya mhusika kupewa cheti/transcript yake.

  1. Mhusika Kama atahitaji kuchukua transcript, atatakiwa kulipia shilingi 10,000/- (kwa kila transcript moja atakayochukua) kwenye akaunti ya benki ya chuo, iliyopo CBRD bank, jina: Tanzania Public Service College, namba 01J1019909102. Hii ifanyike kabla hajaja chuoni.
  2. Mhusika akifika chuoni ajaze “clearence form” inayopatikana hapa chuoni
  3. Muhusika anatakiwa kupeleka risiti ya Benki kwenye ofisi za Uhasibu kwa ajili ya kuingizwa kwenye mfumo wa uhasibu wa chuo, ambapo atapewa risiti mpya toka chuoni
  4. Kwa kutumia risiti mpya ya chuo, mhusika atafika ofisi za masijala kuchukua cheti au transcript yake. Na kama kama kuna makosa atatoa taarifa kwenye ofisi ya usajili ya chuo.
  5. Kwa wale wanaowachukulia wengine, hakikisha unayemchukulia amekupa barua ya kukutambulisha, risiti ya bank iliyoelezwa hapo juu (kama unamchukulia transcript), clearance form na kopi ya kitambulisho chako (wewe nayemchukulia mwenzako).

KUMBUKA HATUPOKEI FEDHA TASLIMU HAPA CHUONI, FEDHA ZOTE ZILIPWE BENKI YA CRDB KA AKAUNTI ILIYOTAJWA